SIMBA YATOSHANA NGUVU NA KIKOSI CHA MWENGE


Na,Said Ally
Timu ya soka ya Simba imeshindwa kuchomoza na ushindi mbele ya kikosi cha timu ya Mwenge baada ya kulazimishwa sale ya 1-1 katika mchezo wa kombe la Mapinduzi inayoendelea kufanyika hapa Zanzibar.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani wa hali ya juu kwa timu zote,Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza goli ambalo limefungwa na mchezaji Jamali Mwambeleko kunako dakika ya pili ya mchezo.

Baada ya goli hilo Simba iliendelea kuliandama lango la wapinzani wao lakini ukosefu wa umakini katika safu ya ushambuliaji iliwafanya wekundu hao kushinda kupachika bao lingine.

Kwa upande wao Mwenge ambao awali ilionekana kana kwamba wangekumbana na idadi kubwa ya magoli ilianza kubadilika katika kipindi hicho cha kwanza kwa kucheza kwa maelewano na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha lililofungwa na Humud Abraham katika dakika ya 29 ya mchezo.

Hadi kipindi cha kwanza kinakamilika timu hizo zilifungana bao 1-1.

Kipindi cha pili Simba ilifanya mabadiliko ya wachezaji wa nne ambao kocha Masoud Djuma aliwatoa Juma Luizio,Jamali Mwambeleko,Moses Kitandu na Ally Shomari ambapo nafasi zao zilichukuliwa na John Boko,Shiza Ramadhani Kichuya,Nicholas Gyan na Kevin Faru lakini mabadiliko hayo hayakuweza kubadili taswira ya mchezo katika 90 za mtanange huo ambao ulimalizika kwa kufungana bao 1-1.

Baada ya mchezo huko kukamili,kocha wa timu ya Simba,Masoud Djuma amesema kwamba malengo yake yalikuwa n kupata ushindi katika mchezo wa kwanza lakini jambo hilo limeshindikana hivyo kwa sasa anaendelea kukifanyia kazi kikosi chake ili kiweze kufanya vizuri katika michezo mingine kwani bado wana nafasi.

Kwa upande wake kocha wa timu ya Mwenge,Musa Salim yeye amewapongeza wachezaji wake kwa kucheza kwa juhudi na maalifa akisema kwamba Mwenge ya sasa iko vizuri na anaamini itafanya makubwa zaidi katika mashindano hayo ya kombe la mapinduzi.


No comments