KOCHA URA AKATAA TIMU YAKE KUCHEZA NA YANGA KWENYE MAPINDUZI CUP

Na,Said Ally,Zanzibar
Kocha msaidizi wa timu ya URA ya nchini Uganda Kalanzi Hamza amesema kwamba Yanga ndio timu ambayo anaihofia katika michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea kufanyika hapa Zanzibar.

Hamza ameiambia Mwandike.BLOGSPOT,kwamba amepata nafasi ya kuzishuhudia timu zote ambazo zinashiriki michuano hiyo ikiwemo Simba na Azam FC lakini amebaini kuwa Yanga ina kikosi bora ambacho kinacheza mfumo kama wa timu yake.

"Yanga wanajua kucheza,wanacheza sawasawa kama sisi tunavocheza,mimi nasema sitaki wanipatie hiyo Yanga,jua Yanga saa yoyote wanaweza kunipiga ama mimi naweza kuwapiga"alisema Hamza.

Hata hivyo alisema kwamba kwa kuwa wamekuja kushiriki katika michuano hiyo ya kombe la Mapinduzi kwao wako tayari kukutana na timu hiyo ya Yanga endapo kama watakutana nao.,,,

Kwa taarifa zaidi tegea 98.1 Wapo Radio FM,kuanzia saa 12 na nusu jioni hadi saa moja katika kipindi cha Duru za michezo.

No comments