SIMBA WASEMA WAPO KAMILI KWA MAPINDUZI CUP

Na Said Ally,Zanzibar
Uongozi wa timu ya soka ya Simba umesema kwamba kikosi chao kimejipanga vyema kuikabili timu ya Mwenge hapo kesho katika mchezo wao wa michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea kufanyika hapa visiwani Zanzibar.

Mratibu wa timu ya Simba,Abasi Ally alisema kwamba wamekuja Zanzibar kwa lengo la kupambana na malengo yao ya kwanza ni kushinda katika mechi zote katika mashindano hayo.

Alisema kwamba kikosi kamili kimewasili Zanzibar akiwemo mchezaji wao aliyesajiliwa katika dirisha dogo la usajili Asante Kwasi hivyo benchi la ufundi lina wigo mpana wa kuamua atakaecheza katika mchezo husika.

Simba inataraji kushuka katika uwanja wa Amani mishale ya saa 10 kamili jioni ambapo mapema kabla ya mchezo huo Singida United itamenyana na Zimamoto saa nane mchana huku mechi ya mwisho kwa siku ya kesho itazikutanisha Yanga na timu ya Mlandege,mchezo unaotarajiwa kupigwa mishale ya saa mbili na robo.

No comments