KOCHA JKU ASEMA WAAMUZI WAMEIBEBA YANGA

Na Said Ally,Zanzibar
Kocha mkuu wa timu ya JKU,Ally Sleiman Mtuli amewalaamu waamuzi ambao wamechezesha mchezo wao wa kombe la Mapinduzi dhidi ya Yanga akisema kwamba wameshindwa kutafasiri vyema sheria 17 za soka.

Mtuli alisema kwamba katika mchezo huo ambao walipoteza kwa kufungwa kwa jumla ya goli 1-0,bao ambalo limefungwa na mchezaji Hassan Ramadhani Kessy kunako dakika ya 90,Yanga ilipaswa kucheza pungufu kutokana na faulo ambazo wamezifanya.

Alisema kwamba wachezaji wa Yanga walifanya makosa mengi ya kiuchezaji kwa kucheza faulo nyingi lakini waamuzi hao wameshindwa kulitambua jukumu lao la kufuata sheria 17 za soka.

Aidha alisema kwamba kufungwa kwao katika mechi hiyo katika dakika za mwisho kumewaumiza zaidi kwani wachezaji wake walicheza kwa juhudi na maarifa tangu mwanzo wa mchezo huo ambao ulikiwa na ushindani wa hali ya juu ya kwa pande zote.

JKU baada ya kupoteza katika mchezo huo inaendelea kushika nafasi ya nne katika msimamo wa kundi B wakiwa na alama nne baada ya kucheza michezo minne kwenye mashindano hayo ya kombe la Mapinduzi.

No comments