SIMBA YAREJEA KILELENI KWENYE MSIMAMO WA LIGI KUU YA TANZANIA BARA


Na Said Ally
Timu ya soka ya Simba imefanikiwa kurejea kileleni katika msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara baada ya leo hii kufanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2-0 mbele ya Kagera Sugar katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Simba imepata ushindi huo kupitia kwa wachezaji wake Said Ndemla na John Boko ambapo magoli hayo yote yamepatika katika kipindi cha pili cha mchezo huo uliokuwa na ushindani zaidi hasa katika kipindi cha kwanza huku beki Shomari Kapombe aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu akitoa pasi ya goli la pili.

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha jumla ya alama 32 na kurejea kileleni katika msimamo wa ligi baada ya kushuka dimbani katika michezo 14.

Nafasi ya pili inashikiliwa na Azam FC wenye alama 30 wakifuatiwa na Yanga katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 25,timu zote hizo zikiwa zimeshacheza mechi 14.

No comments