YANGA WASEMA HAYA BAADA YA AZAM FC KUTANGAZA MECHI YAO KUCHEZWA SAA MOJA
Na,Said Ally
Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kwamba una taarifa kutoka TFF kuwa mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Azam FC,utachezwa mishale ya saa 10 kamili jioni katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi.
Msemaji wa timu ya Yanga,Dismas Ten amieambia Saidallymwandike.blogspot.com kwamba wao kama uongozi wana taarifa ya mechi hiyo itakayochezwa siku ya jumamosi kuanza mishale ya saa kumi jioni licha ya uongozi wa Azam FC kupitia kwa msemaji wao kudai kuwa mchezo huo utapigwa saa moja usiku.
"Hakuna jambo baya kucheza,tushacheza mechi nyingi usiku ndani na nje ya nchi, kwa hiyo kwetu sisi sio jambo geni lakini taarifa iliyopo ni kwamba mchezo utachezwa jioni saa 10, tuna taarifa kutoka shirikisho"alisema Ten.
Alisema kwamba kama kutakuwa na mabadiliko ya muda kwao hawatakuwa na tatizo kwa kuwa wamejipanga kucheza muda wowote ule utakaopangwa.
Aidha katika hatua nyingine alisema kwamba kikosi cha timu hiyo kinaendelea na mazoezi kikiwa jijini Dar es salaam kwa ajili ya kujiwinda na pambano hilo la ligi kuu ya Tanzania bara huku pia akidai kuwa jambo la faraja ni kuona wachezaji wote wakifanya mazoezi ispokuwa Donald Ngoma ambae ni mgonjwa.

Post a Comment