KOCHA RUVU SHOOTING ASEMA WAAMUZI WAMEIBEBA YANGA
Na,Said Ally
Kocha mkuu wa timu ya Ruvu Shooting,Abdulmutik Haji maarufu kwa jina Kiduhu amelaumu maamuzi ya mwamuzi Florentina Zabron kutoka mkoani Dodoma baada ya kusema kwamba ameshindwa kufuata sheria 17 za soka katika mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Yanga.
Kiduhu ameiambia Saidallymwandike.blogspot.com kwamba waamuzi wa mechi yao dhidi ya Yanga wameshindwa kutafasiri vyema sheria 17 za soka hasa kutokana na maamuzi yao ya makosa ambayo wameyatoa uwanjani katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kusabisha timu yake kukubali kichapo cha bao 1-0.
"Pafomensi ya waamuzi ilikuwa pua,ukiangalia tumepata penati klia kaikataa,hata goli lile ambalo tumefungwa ule mpira kautoa mchezaji wao lakini kaenda kuweka kona tukaukumiwa goli,mambo mengi yalikuwa yanatuenea lakini ndio timu kubwa kwa hiyo tunaenda hivyo hivyo kitimu kubwa kubwa"alisema Kiduhu.
Hata hivyo alisema kwamba kwa sasa wanarejea nyumbani kwa ajili ya kujipanga na michezo mingine ambayo imesalia ya ligi kuu ya Tanzania bara hivyo anaamini kikosi chake kitafanya vizuri katika michezo hiyo kwani mechi nyingi watacheza wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Post a Comment