MTOTO WA RAY AWA GUMZO KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Na Said Ally
Mtoto wa staa wa bongo Movie Vicent Kigosi "Ray" amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya picha za mtoto huyo kuenea katika mitandao hiyo

Mastaa mbalimbali hasa wa bongo Movie walimpost kwenye kurasa zao za instagram wakimtakia Happy birthday na kumtakia maisha marefu mtoto huyo anaejulikana kwa jina la Jaden aliyetimiza mwaka mmoja.

Miongoni mwa mastaa hao ni pamoja Wema Sepetu ambae yeye alionekana zaidi kumsifia mtoto huyo kutokana na uzuri wake.

"Kuna watu wana machango bwana...CHUCHU....!!!! CHUCHU...!!!! nakuita tena CHUCHU...!!!! una Chango baby...MASHALLAH...nilivyoiona hii picha nilifumbua macho tena yawe makubwa zaidi ili niweze kuona vizuri...Haka katoto ni Kashweeeeet...!!!! Kashweet mpaka kashweet tena...ila mtoto raha sana jamani...Raha mnoooo...!!!! Huyu ukiwa nae ndani analia lia hata kula hutaki...Happy Birthday Lil baby angel..cc"aliandika wema kupitia ukurasa wake wa instagram.

Mbali na Wema pia wasanii mbalimbali wamemsifia mtoto huyo huku baadhi yao wakisema kwamba Jaden amewafunika watoto wengi wa mastaa wa bongo.


No comments