TFF WAMTANGAZA KOCHA WA KILIMANJARO STARS

Ammy Conrad Ninje, ametangazwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwamba ndiye atakuwa Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ itakayoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji mwaka huu wa 2017.
Katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Desemba 3, mwaka huu, Kilimanjaro Stars imepangwa Kundi ‘A’ pamoja wenyeji Kenya, Rwanda na Libya ambayo ni timu mwalikwa kutoka Kaskazini mwa Afrika.
Ninje ambaye kikosi chake atakitangaza kesho Jumamosi Novemba 18, 2017 alitambulishwa na Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas katika mkutano na wanahabari uliofanyika Ukumbi wa Hosteli za TFF, Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Kilimanjaro Stars ambayo imewahi kutwaa mara tatu taji hilo la Chalenji tangu kuanzishwa kwake, itaaza kampeni za kurudisha heshima yake dhidi ya Libya katika kundi hilo la A utaofanyika Desemba 3, mwaka huu.
Wasifu wa Ammy Ninje
Ammy Conrad Ninje alizaliwa mwaka 1978, Dar es Salaam, Tanzania na alianza shule msingi Bunge iliyopo Jiji Kuu la Tanzania,  kuanzia mwaka 1985 – 1991.
Alisoma shule ya Sekondari ya Kilimanjaro 1992 na baadaye alijiunga kidato cha tano na sita Shule ya Sekondari ya Al-Haramain, Kariakoo jijini.

Alianza kucheza soka katika timu ya Boom FC ya Ilala na baadaye Manyema FC zote za Dar es Salaam kabla ya kujiunga JKT Ruvu wakati huo inaitwa 832 KJ Ruvu.

Baadaye alikwenda kucheza soka Afrika Kusini kwenye timu za Hellenic FC na kisha Wynberg St Jones kabla  ya kujiunga na Sparta Rotterdam (Mutual) FC ya China pia alicheza katika nchi za Denmark, USA, Scotland na England.

Amewahi kucheza timu ya Taifa ya Tanzania katika vipindi tofauti wakati inafundishwa na Kocha mzawa Profesa Mshindo Msolla.

Alianza kufundisha soka katika chuo cha Hull 2007-2010
Hull City FC 2008-2013
Collingwood Primary School 2009-2013
Soccer for all 2012-2014 na
Notts County FC  tangu 2013 hadi sasa.
Nje ya mpira wa miguu kama mwalimu na kabla mchezaji, kwa sasa anasomea uhasibu.
Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.

No comments