AFANDE SELE AELEZA MAZITO YA KANUMBA KUHUSU LULU
Na Said Ally
Msanii wa muziki wa hip hop na bongo flava kutoka mkoani Morogoro Seleman Msindi maarufu kwa jina "Afande Sele"ametoa ujumbe mzito kwa watanzania unaomuhusu msanii wa maigizo Elizabeth Michael "Lulu"ambae leo hii amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusidia.
Afande Sele kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika ujumbe mrefu wenye sehemu mbili unaolezea jinsi msanii huyo alivyomfahamu Lulu tangu akiwa mdogo hasa baada ya kukutana nae usiku wa manane kwenye ukumbi wa Dar west uliopo Tabata mwaka 2006.
Katika ujumbe huo Afande Sele ametoa lawama kubwa kwa marehemu Stivin Kanumba akisema kwamba yeye ni sehemu ya watu walioharibu maisha ya Lulu kwa kushindwa kutambua thamani ya mtoto kwa kipindi alichokuwa nae.
Alisema kwamba Kanumba ni mtu mbaya sana, alifanya kitendo kibaya dhidi ya binti mdogo aliyepaswa kumsaidia kufikia malengo na sio kumtumia kwa sababu ya umaarufu wake.
Aliongeza kwa kuandika kuwa Kanumba amevuna alichopanda lakini Lulu unyonge wa kiumri na udhaifu wa kisichana vimebakia kuwa mateso katika maisha yake lakini kwa upande wa Kanumba anaamini mungu amempa haki ya matendo yake mabaya kwa kumlaza mapema.

Post a Comment