TFF WAKANUSHA TAARIFA INAYOSAMBAA MITANDAONI
Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF leo hii limetoa ufafanuzi kuhusiana na tuhuma ambazo zinalikabili shirikisho hilo juu ya ongezeko la matumizi ya fedha kwa uongozi mpya ulioingia madarakani.
Katibu mkuu wa TFF,Wilfred Kidao leo hii amezungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na jambo hilo ambapo ameeleza kuwa taarifa hizo si za kweli ambazo zina lengo la kuichafua TFF.
Kidao alisema kwamba kamati ya utendaji ya TFF haijawai kujadili kuhusu posho za vikao wala kuengeza posho za vikao kama ambavyo inaelezwa kupitia taarifa inayosambaa kwenye mitandao.
Alisema kwamba kamati ya utendaji ilikubaliana kwa pamoja kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji alipwe kiasi kisichozidi shilingi milioni moja na nusu katika miezi mitatu.
Aliongeza kuwa fedha hizo zitalipwa kwa mjumbe aliyebainika kufanya kazi katika kanda yake kupitia lipoti atakayowasilisha kwenye kikao cha kawaida cha kamati ya utendaji.
Aidha alisema kwamba Rais wa TFF,Wallace Karia na makamu wake wamekataa kulipwa fedha ambazo wajumbe wa kamati ya utendaji walipendekeza viongozi hao wajuu nao waweze kulipwa kutokana na kazi wanazozifanya.
Hata hivyo alisema kwamba Rais ameandika waraka kwa wajumbe hao akisema kwamba kwa sasa si kipindi cha yeye kulipwa fedha bali fedha hizo ni vyema zikalekezwa kwenye maendeleo ya soka hadi hapo shirikisho hilo litakapojimudu kuichumi.
TAARIFA AMBAYO IMETOLEWA UFAFANUZI NA KATIBU MKUU NI HII HAPA CHINI
🔴 *TFF KWAANZA KUFUKUTA MAPEMAAA.....*♂♂♂♂♂♂♂
*KAMATI TENDAJI YA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) KUTUMIA MILIONI 438 KWA MWAKA KUJILIPA POSHO*.
Tarehe 28/10/2017 Kamati ya Utendaji ya TFF, ilifanya Kikao katika Hoteli ya SEA SCAPE Kunduchi Beach jijiji Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine ilipitisha azimio la Wajumbe wa Kamati hiyo kuanza kulipwa posho ya kila mwezi kwa mchanganuo ufuatao:
1. Rais wa TFF Tsh.Mil.6 kwa mwezi sawa na Mil.72 kwa Mwaka.
2. Makamu wa Rais wa TFF, Tsh. mil. 5 kwa mwezi sawa na Mil.60 kwa mwaka.
3. Wajumbe 20 wa Kamati ya Utendaji kila mmoja Tsh. Mil. 1 kwa mwezi sawa na mil.12 kwa mwaka , kwa wajumbe 20 ni Tsh. Mil. 240 kwa mwaka.
2. Makamu wa Rais wa TFF, Tsh. mil. 5 kwa mwezi sawa na Mil.60 kwa mwaka.
3. Wajumbe 20 wa Kamati ya Utendaji kila mmoja Tsh. Mil. 1 kwa mwezi sawa na mil.12 kwa mwaka , kwa wajumbe 20 ni Tsh. Mil. 240 kwa mwaka.
NB: Posho hizi ni mpya na hazijawahi kuwepo katika shirikisho hilo katika uongozi uliopita.
Aidha Posho za kila kikao zimepanda kutoka Tsh. 300, 000/= uongozi uliopita hadi laki tano (500,000/) uongozi wa sasa kwa kila mjumbe, kwa mwaka kuna vikao vya kawaida visivyopungua sita, kwa Wajumbe wote 22 kwa mwaka itakuwa mil.66.
Kwa mchanganuo huo, Gharama za Posho tu kwa mwaka kwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji tu ni milioni mia nne thelathini na nane (mil.438). Bado posho za vikao vya dharura, posho za watumishi wengine n.k
*Moja ya changamoto za maendeleo ya Mpira wa Miguu Tanzania ni Ukosefu wa fedha.* *Timu zetu za taifa zinashindwa kukaa kambini, Waamuzi wanakosa Mafunzo, viwanja vya michezo vinashindwa kuboreshwa, vilabu vya michezo havisaidiwi na mambo mengine chungu nzima hayafanyiki sababu ya ukosefu wa fedha, leo hii EXCOM inakwenda kujifungia Sea ESCAPE na kuidhinisha mil. 438 kwa ajili kujilipa posho! Kwa mwendo huu tusitegemee maendeleo katika soka Tanzania. Rais wa TFF, WALES KARIA na Makamu wake, MICHAEL WAMBURA wanapaswa kujitathmini upya.*
Post a Comment