MTIBWA SUGAR HAWANA TAARIFA ZA MCHEZJI WAO KUSAJILIWA NA YANGA

Uongozi wa timu ya soka ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani mkoani Morogoro umesema kwamba hauna taarifa zozote zinazomuhusu mchezaji wao Mohamed Issa maarufu kwa jina la Banka kutakiwa na klabu ya Yanga.

Msemaji wa timu hiyo Thobias Kifaru alisema kwamba kwa upande wao kama uongozi hawana taarifa hizo kwani mchezaji pia bado ana mkataba na wakata miwa hao wa Manungu.

Alisema kwamba kwa kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo kuna mengi yatazungumzwa lakini kwao hawana wasi wasi na tetesi hizo ambazo zinazungumzwa.

No comments