TAIFA STARS YAREJEA NCHINI



Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kimerejea usiku wa kuamkia leo hii kikitokea nchini Benin kilipokwenda kushiriki mchezo wa kimataifa wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya FIFA dhidi ya Benin.

Afisa Habari wa TFF,Alfred Lucas alisema kwamba baada ya kuwasili hapa nchini baadhi ya wachezaji wameelekea kambini katika timu zao huku wekingine wameelekea nyumbani kwao kabla ya kuungana na timu zao kwa ajili ya kushiriki michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara.

Lucas alisema kwamba kwa wachezaji wa Simba na Prisons wao moja kwa moja TFF iliamua kuwasafirisha mapema ili wakajiunge na timu zao kutokana na makubaliano ambayo wamekubaliana na viongozi wao.

No comments