MOHAMMED ISSA "BANKA"AUNGANA RASMI NA TIMU YA TAIFA

Na Sleiman Ussi,Zanzibar
Kiungo Mshambuliji wa Mtibwa Sugar Mohammed Issa "Banka" ameungana na wenzake kwenye mazoezi ya timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes).

Banka alisema kwamba amejiunga na timu hiyo ya Taifa baada kuruhusiwa na uongozi wa timu ya Mtibwa Sugar na hii inatokana na yeye kutokuwa na nafasi ya kucheza katika mchezo wao ujao dhidi ya Kagera Sugar kutokana na kukabiliwa na kadi tatu za njano.

Banka anakuwa mchezaji wa pili kutoka ligi kuu soka Tanzania Bara kujiunga na kikosi hicho akitanguliwa na mshambuliaji wa Majimaji Suleiman Kassim "Seleembe"


No comments