YANGA YATOA MSIMAMO WAO JUU YA MWAMUZI WA MECHI YA KESHO

Baada ya kamati ya waamuzi kumteua mwamuzi Mathew Akrama wa Mwanza kuchezesha pambano la watani wa jadi Simba na Yanga hapo kesho,uongozi wa klabu ya Yanga umetoa tahadhari kwa mwamuzi huyo kuchezesha pambano hilo kwa kufuata sheria 17 za soka.

Mkwasa alisema kwa upande wao wamekuwa na mshangao mkubwa kuhusu mwamuzi huyo kwani taarifa za kuteuliwa Akrama zimefahamika toka jana huku wapinzani wao Simba wakiwa na majina ya waamuzi hao.

Alisema kwamba Yanga inaheshimu maamuzi ya kamati hiyo lakini ni vyema haki ikatendeka katika kutafasiri sheria 17 za mpira wa miguu kwani mwamuzi huyo awali alishindwa kumudu mpambano kama huo wa watani wa jadi uliochezwa mwaka 2012 na timu hizo kutoka sale ya bao 1-1 huku winga Saimon Msuva akizawadiwa kadi nyekundu.

No comments