MASAU BWIRE AWAPONGEZA VIJANA WA SIMBA

Baada ya timu ya vijana ya Simba kufanikiwa kuwa mabingwa wa michuano ya vijana iliyoandaliwa na TFF,wadau mbalimbali wa mpira wa miguu hapa nchini akiwemo msemaji wa Ruvu Shooting wamekipongeza kikosi cha timu hiyo kwamba kwa kiwango ambacho wamekionyesha kwenye mechi zao,timu hiyo imestahili kuwa bingwa.

Masau Bwire amesema kwamba kwa upande wake ameridhishwa na kiwango cha timu ya Simba na amediliki kusema kwamba ni vyema mafunzo wanayoyapata wachezaji wa timu hiyo yakapelekwa kwa timu ya wakubwa.

No comments