YANGA YAFUNGA USAJILI KWA KUWANASA NYOTA WAWILI

Wakati zoezi la usajili wa dirisha dogo likitaraji kufungwa rasmi leo hii ifikapo mishale ya saa sita usiku,uongozi wa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara,timu ya soka ya Yanga,umesema kwamba leo hii umekamilisha zoezi la usajili wa dirisha dogo kwa kuongeza wachezaji wawili ambao ni kiungo kutoka Zambia Justine Zulu pamoja na msahambuliaji Emmanuel Martine aliyekuwa anaitumikia timu ya JKU ya Zanzibar.

Kaimu katibu mkuu wa klabu hiyo Baraka Deusdedit ameiambia MWANDIKE BLOGSPORT kwamba wachezaji hao wawili ndio ambao wataungangana na wachezaji wengine kwa ajili ya kujiandaa na michuano mbalimbali ikiwemo ya ligi kuu ya Tanzania bara.

Baraka amesema kwamba pia ndani ya kikosi cha timu hiyo hakuna mchezaji yeyote aliyeachwa au kupelekwa kwa mkopo zaidi ya Mbuyu Twite aliyemaliza mkataba wake.

Hata hivyo amedai kuwa kwa sasa kikosi kinaendelea vizuri na maandalizi kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya jumamosi dhidi ya JKT RUVU itakayopigwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

No comments