SERIKALI YATAKIWA KUWA MAKINI NA USIMAMIZI WA MFUMO MPYA WA TIKETI

Serikali kupitia kwa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo imetakiwa kusimamia vyema swala zima la mfumo wa tiketi za mtandao ambazo zimekuwa zikitumika katika michezo ya ligi kuu Tanzania bara na mechi mbalimbali.

Mmoja wa wanachama wa klabu ya Yanga Hossein Mohemed amesema kwamba serikali inatakiwa kuisimamia vyema kampuni iliyopewa tenda ya kuratibu mfumo huo kwani inaonyesha hawakujiandaa kikamilifu.

Amesema kwamba mfano mzuri ni katika mechi iliyochezwa siku ya jumamosi kati ya Yanga na JKU ambapo amedai kuwa tiketi hizo zimeshindwa kumudu kufanya kazi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa mashabiki ambao kwa kiasi kikubwa walijitokeza uwanjani kushuhudia mechi hiyo ya kirafiki.

No comments