SIMBA WAWEKA BAYANA JUU YA USAJILI WA JUMA LUIZIO

Uongozi wa klabu ya Simba umeweka bayana juu ya taarifa za  usajili wa mchezaji Juma Luizio kutoka klabu ya Zesco ya nchini Zambia ambapo wekundu hao wana mpango wa kumsajili kwa njia ya mkopo.

Makamu wa Raisi wa Simba,Godfrey Nyange Kaburu amesema kwamba uongozi utaweka bayana usajili wao hapo kesho pale dirisha litakapofungwa.

Amesema kwamba kwa sasa wana mapendekezo ya kusajili washambuliaji wawili wa hapa nyumbani hivyo swala hilo linakamilishwa na hii inatokana mara baada ya mchezaji Ame Ally kuondoka kwenye timu hiyo.

Hata hivyo amedai kuwa hata taarifa za kuachwa kwa mlinda malango wao namba moja Vicent Angban nazo zitatolewa taarifa hapo kesho.

No comments