NDANDA WASUBIRI RIPOTI YA MWALIMU KUAMUA HATMA YA OMARY MPONDA

Uongozi wa timu ya soka ya Ndanda ya mkoani Mtwara umesema kwamba taarifa zote za usajili wa klabu hiyo wanataraji kuzipata mwishoni mwa wiki kutoka kwa benchi la ufundi la timu hiyo mara baada ya ligi kumalizika kwa mzunguko wa kwanza.

Afsa Habari wa Ndanda Idrisa Bandali amesema kwamba baada ya kupokea taarifa hizo ndipo watafahamu juu ya wachezaji watakaongezwa au watakaoachwa katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili lililofungulia rasmi hapo juzi.

Bandali amesema kwamba hata swala la mchezaji Omary Mponda anaeidaiwa kujiunga na klabu ya Simba kwa upande wao kama uongozi hawana taarifa hizo ispokuwa uongozi utakuwa tayari kufanya mazungumzo na timu yeyote yenye nia ya kusajili mchezaji wa timu hiyo.

No comments