TASMA WAWAPONGEZA WACHEZAJI WA LIGI KUU

Chama cha madaktari wa tiba za michezo hapa nchini Tasma kimewashukuru wadau wa mpira wa miguu pamoja na wanamichezo kwa ujumla kwa kufanikisha mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Tanzania bara unamalizika pasipo kuwa na dosari kubwa kwenye swala la afya ya wachezaji hasa kwenye ushiriki wao kwenye michezo ya ligi.

Katibu mkuu wa chama hicho Nassoro Ally Matuzya amesema kwamba kwa upande wao kama TASMA hawana budi kuwapongeza wachezaji kwa kucheza mchezo wa kiungwana hadi mzunguko wa kwanza unamalizika.

No comments