MWADUI MBIONI KUZIBA PENGO LA JULIO

Baada ya kushindwa kufanya vizuri katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Tanzania bara,uongozi wa timu ya Mwadui ya mkoani Shinyanga umesema kwamba kwa sasa wanataraji kufanya maboresho ya kikosi ili kifanikiwe kufanya vizuri mzunguko wa pili.

Katibu mkuu wa Mwadui Ramadhani Kilao amesema kwamba jambo la kwanza ambalo linatarajiwa kufanyiwa maboresho ni juu ya kocha mkuu kwani tangu kujiuzulu kwa Jamhuri Kiwelu Julio hawajafanikiwa kupata mrithi wake.

Kilao amesema kwamba kwa sasa wapo kwenye mazungumzo na baadhi ya makocha mbalimbali hapa nchini na kwa kiasi kikubwa makocha hao wameonyesha dhamira ya kujiunga na timu hiyo kutoka mkoani Shinyanga.

No comments