AZAM B KUANZA NA MBAO FC KATIKA LIGI YA TAIFA YA VIJANA
Timu ya vijana ya Klabu Bingwa ya Afrika
Mashariki na Kati Azam FC ‘Azam U-20’, kesho saa 8.30 mchana inatarajia kuanza
kutupa karata ya kwanza kwenye Ligi ya Taifa ya Vijana kwa kukipiga dhidi ya
Mbao katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, mkoani Kagera.
Azam
U-20 iliyojiandaa vema kuelekea michuano hiyo, imepangwa kwenye kituo cha
Bukoba chenye timu nane kinachounda Kundi A, kikiwa na timu nyingine za Kagera
Sugar, Toto African, African Lyon, Mwadui, Stand United na Yanga.
Akizungumza
na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Idd
Cheche, alisema kuwa wamejipanga vilivyo kuanza vema michuano hiyo kwa kupata
ushindi kesho.
“Kikosi
changu kipo kamili kwa ajili ya michuano hiyo, kimefanya maandalizi mazuri na
malengo yetu makubwa ni kumaliza nafasi ya kwanza kwenye kituo hiki na hatimaye
kuibuka mabingwa,” alisema.
Cheche
aliwatoa hofu mashabiki wa Azam FC kwa kuwaaambia kuwa wakae mkao wa kula
kutokana na ubora wa timu yao na ipo vizuri kwa ajili ya kushindana na hatimaye
kutwaa ubingwa.
Mabingwa
hao wa kihistoria wa michuano ya awali ya vijana ya Uhai Cup, wanatarajia
kung’arishwa vilivyo na baadhi ya mastaa wake wakiwemo mshambuliaji Shaaban Idd
na kiungo Masoud Abdallah, ambao pia wamepandishwa kucheza kwenye timu ya
wakubwa ya kikosi hicho.
Tayari mchezo wa ufunguzi wa kituo hicho umefanyika jana, ambapo
ilishuhudiwa Kagera Sugar ikitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Yanga huku leo Jumatano
ukitarajiwa kupigwa mtanange mwingine utakaohusisha watani wa jiji la
Shinyanga, Stand na Mwadui.
Post a Comment