KAMATI YA RUFAA YA TFF YAFUTA MCHAKATO WA UCHAGUZI WA IRFA


Kamati ya rufaa ya shirikisho la soka tanzania TFF imetolea maamuzi juu ya rufaa mbili ambazo zimekuwa zikipinga maamuzi ya kamati ya rufaa ya chama cha soka cha mkoa wa iringa kupitisha baadhi ya majina ya wagombea.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa wa kamati ya rufaa ya TFF Dr. Mutabazi Julius Lugazia amesema kwanza  wamepokea rufaa mbili ambazo moja imekatwa na FESTO MKEMWA juu ya kupitishwa kwa jina la mwenyekiti anayemaliza muda wake Cyprian CHARLES  KUYAVA anagombea nafasi ya uenyekiti.


Rufaa ya pili imekatwa na Ramadhani Marko Muhona ikipinga maamuzi ya kamati ya uchaguzi mkoa wa iringa kwa kupitisha jina la ABUU SUFIAN kuwa  mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF.


Mwenyekiti wa kamati ya rufaa ya TFF lugazia amesema kutokana na dosari ambazo zimejitokeza katika mchakato mzima wa uchaguzi  kamati imeamaua kuufuta mchakato wa uchaguzi wa chama cha soka cha iringa na kutoa siku kumi na nne zoezi la kurudia uchaguzi kuwa limekamilika.

No comments