YONDANI AVURUGA MIPANGO YA MKWASA



Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imeondoka leo hii kuelekea nchini Nigeria kwa ajili ya kushiriki mchezo wa kukamilisha ratiba wa kufuzu kwa fainali za Afrika.

Ofsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba Stars imesafiri kwa shirika la ndege la Ethiopia ambapo wachezaji wote walioitwa na kocha mkuu Chars Boniphace wameambatana ispokua mchezaji mmoja Cavin Yondani ambae ameshindwa kuungana na timu huku sababu za kukosekana kwake kutojulikana.

Lucas amesema kwamba kocha mkuu wa timu hiyo amehudhunishwa na swala hilo la kukosekana kwake Yondani kwani mara nyingi amejalibu kufanya nae mawasiliano lkn kwa njia mbalimbali ikiwemo kumtumia meseji lkn hakujibu.

Amesema kwamba mbali na kufanya nae mawasiliano lakini pia wakajalibu kuzungumza na kaimu katibu mkuu wa klabu ya Yanga,Baraka Deusidedit ili kufahamu swala la mchezaji huyo kutoungana na wenzake ambapo katibu huyo amesema kwamba hata kambini kwa klabu hiyo hayupo baada yay eye mchezji kutoa taarifa kua ana matatizo ya kifamilia.

Hata hivyo Lucas amedai kua,TFF itachukua hatua mara baada ya kupata ufafanuzi kutoka kwake mchezaji husika kwani huenda nae akakumbwa na matatizo pasipo watu kufahamu hivyo ni vyema kwanza kufahamu maelezo yake kabla ya kutoa maamuzi.

Si unajua hua binadamu tumeumbwa kua na matatizo labda huenda akakumbwa na matatizo ya kifamilia na watu wasijue,mfano mzuri mlinda mlango wa Yanga Deogratius Munishi amekua akidaka mechi mbalimbali za ligi huku mzazi wake akiwa ni mgonjwa,kwa hiyo si vyema kutoa maamuzi kabla ya kupata maelezo "alisema Lucas".

No comments