MANJI AUNGANA NA WADAU WA SOKA KUAGA MWILI WA BABA YAKE DIDA


Mwenyekiti wa klabu ya Yanga,Yusuph Manji leo hii ameungana na wadau wa soka kwa ajili ya ushiriKI wa kuaga mwili wa baba yake mlinda mlango wa klabu hiyo,Deogratius Munishi alimaarufu "DIDA"

Manji amejitokeza katika kanisa  Katoliki Temeke Mikoroshini ambapo mwili wa Munishi Boniventura uliagwa na wadau wengi wa soka wakiwemo wa Yanga na Simba.

Makamu wa Raisi wa klabu ya Simba Geofrei Nyange Kaburu nae alikuwepo kwenye msiba huo sambamba na baadhi ya viongozi mbalimbali wa timu za ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments