MWAMBUSI ARIDHISHWA NA MATOKEO YA MECHI YA KWANZA


Kocha msaidizi wa timu ya soka ya Yanga,Juma Mwambusi amesema kwamba amefurahishwa na matokeo ya mechi yao ya kwanza ya ligi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Afrika Lyon katika mechi ambayo imechezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mwambusi amesema kwamba ushindi ambao wameupata leo hii ni ushindi muhimu kwa upande wao kwani utawaweka kwenye mazingira mazuri ya kuanza kampeni zao za kutetea ubingwa wa ligi hiyo.

"Matokeo haya ni mazuri sana kwetu ukichukulia tumetoka kwenye mechi za kimataifa na wachezaji wetu wengi ni majeruhi kwa hivyo hili ni jambo la kumshukuru mungu" alisema Mwambusi.

Amesema kwamba baada ya mechi ya jana kwa sasa kikosi kinajipanga vyema kufanya vizuri katika michezo ijayo ili waweze kutetea ubingwa wao wa ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments