KISA SAMATA KOCHA WA GENK AAMUA KUPIGA SIMU TFF


Kocha mkuu wa klabu ya KRC Genk ya nchini Ubeligiji, Peter Maes ambayo anacheza mtanzania Mbwana Samata leo hii ametoa angalizo kwa mara nyingine kwa TFF juu ya swala zima la kufahamu afya ya mchezaji huyo kabla ya kumtumia kwenye mechi ya kesho dhidi ya Nigeria.

Ofsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba Maes leo hii amepiga simu kwa TFF kusisitiza jambo hilo kwa kua Samata ni mchezaji tegemeo kwenye kikosi cha Genk iliyokata tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya uefa ndogo huku yeye akiwa chachu ya mafanikio hayo.

Lucas amesema kwamba kwa mujibu wa kocha huyo amedai Samata alipewa mazoezi ya kumpa nguzu Zaidi ili aiwezeshe Genk kutinga hatua ya makundi na baada ya kukamilisha zoezi hilo mwalimu alikua na mipango ya kumpuzisha kwa muda wa wiki moja hivyo kutokana na jambo hili la kuitwa kwake kwenye timu ya Taifa kunampa wasi wasi mkubwa hasa juu ya afya yake.

Aidha Lucas amedai kua kwa kuthamini  afya ya mchezaji kama wao TFF wamefanikiwa kukamilisha zoezi hilo kupitia kwa madaktari wa timu ambao wameyafanya yale yalisemwa na kocha mkuu wa Genk juu ya kutambua afya ya mchezaji kabla ya mchezo husika.

 "kujua afya kwa binadamu ni muhimu ujue mara nyingi hua sisi tunafanya mambo ya kienyeji mtu hujui afya yako unafanya mazoezi ambayo huenda si salama kwa kwako kwa wakati huo"

No comments