NKOMA APEWA MAJUKUMU YA KUINOA KILIMANJARO QUENS



Mwenyekiti wa soka la wanawake Tanzania,Amina Karuma leo hii amemtangaza rasmi Sebastiani Nkoma kua kocha mkuu wa timu ya Kilimanjaro Quens ambayo inataraji kushiriki michuano ya CECAFA ya mpira wa miguu kwa wanawake inayotaraji kufanyika nchini Uganda septemba 11 mwaka huu.

Karuma amesema kwamba pia jina hilo Kilimanjaro Quens limetamburishwa rasmi leo hii baada ya timu hiyo kuwa na wachezaji watanzania bara pekee ambao watashiriki mashindano hayo huku pia nao Zanzibar wakiwa na timu yao itakayoshiriki michuano hiyo ambayo ni ya kwanza kuanzishwa katika ukanda huu wa CECAFA.

Amesema kwamba maandalizi yako vizuri na kikosi cha timu hiyo kinataraji kuelekea mjini Bukubo siku ya tarehe tano ambapo huko itacheza mechi moja ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya timu ya wanawake ya Burundi ambayo itachezwa siku ya tarehe nane ya mwezi huu.

No comments