VIONGOZI WA JUU WA SIMBA WASOMEWA MAELEZO YA AWALI

Kesi inayowakabili viongozi wakuu wa klabu ya Simba Evans Aveva na Geofrey Nyange Kaburu imeahirishwa hadi Aprili 12 mwaka huu baada ya wakili wa Serikali kutoka TAKUKURU Leornad Swai kuiomba Mahakama airisho fupi kwa kuwa wanatarajia kufanyia mabadiliko ya Shitaka kwa kuongeza mshatakiwa mmoja.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba,Swai alidai kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali baada ya upepelezi wa kesi hiyo kukamilika.

Evans Aveva ambae alilazwa kwa muda mrefu leo hii amehudhuria katika kesi hiyo ya utakatishaji fedha inayowakabili yeye pamoja na Kaburu.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka matano ya uhujumu uchumi ikiwemo kughushi,kuwasilisha nyaraka ya uongo na utakatishaji fedha ambazo ni dola za Marekani (USD) 300,000.

No comments