ANTONIO CONTE ADAI HAOFII CHOCHOTE NDANI YA KLABU YA CHELSEA KWA MATOKEO YASIORIDHISHA.

Na Fredy Reuben
Ligi kuu Nchini Uingereza iliendelea hapo jana kwa michezo kadhaa kupigwa kwenye viwanja tofauti lakini macho na masikio ya wengi yalikuwa yakiutazama mchezo wa London Derby kati ya wenyeji Chelsea walipowakaribisha wabishi Tottenham Hotspur katika dimba la Stamford Bridge. 

Katika mchezo huo Chelsea waliweza kupoteza kwa kufungwa idadi ya magoli 3-1 dhidi ya wageni Tottenham, na kuwafanya Tottenham kupata ushindi kwa mara ya kwanza darajani yapata miaka 28 iliyopita. 

Kwa ushindi huo wa jana Tottenham Hotspur imeenda mbele zaidi wakiwa kwenye nafasi ya nne kwa tofauti ya alama nane dhidi ya Chelsea waliko kwenye nafasi ya tano.

Kwa hali hii Chelsea imeanza kufifisha matumaini ya kupata nafasi nne za juu ili iweze kushiriki michuano inayoiingizia vilabu kiasi kikubwa cha pesa (Uefa Champions League) msimu ujao. 

Licha ya matokeo kutokuwa vizuri kocha mwenye misimamo Muitaliano Antonio Conte amesema hawazi wala haofii kitu chochote na utofauti uliopo kati ya wao na Tottenham ni sawa kabisa na wanastahili kuwepo pale. 

"Sihofii kitu chochote," alisema Antonio Conte, liliripoti Gazeti la The Guardian.

"Nimewapa wachezaji kila kitu. tumekuwa tukifanya kazi kwa nguvu zote kujaribu kuwa na msimu mzuri, lakini mwisho wa siku hadi hapa tulipofikia msimu huu tunastahili. ina maana thamani yetu ndio hii. 

"Nilikuwa na maoni yangu lakini nimechoka kurudia kitu cha aina moja kila uchwao, sihitaji kutengeneza matatizo. kama tupo kwenye nafasi hii, tunastahili kuwepo kwenye nafasi hii.

"Unatakiwa kuiuliza klabu, na sio mimi (kuhusu klabu kumaliza kwenye nafasi nne za juu). narudia tena: Kazi yangu ni kufanya kazi na kazi nafahamu nafanya masaa 24, mimi na benchi langu la ufundi. 

"Kwa wachezaji wangu sina shaka nao wanafanya kazi kwa kiwango cha hali ya juu, licha ya kwamba tupo kwenye nafasi hii, tunatakiwa tuhofie hili." #Niko_Fair

No comments