YANGA YAPANGWA NA SINGIDA UNITED FA CUP

Na Said Ally
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara timu ya soka ya Yanga imepangwa kucheza na Singida United katika mchezo wa robo fainali ya mashindano ya Azam Sport Federation baada ya droo hiyo kufanyika leo asubuhi.

Yanga itawalazimu kusafiri hadi mkoani Singida kwa ajili ya mtanange huo ambao utapigwa kwenye uwanja wa Namfua.

Azam FC wamepangwa kucheza na Mtibwa Sugar,mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex ulioko nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Tanzania Prisons watakuwa nyumbani kuwakaribisha timu ya JKT Tanzania,mchezo ambao unatarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.

Mechi nyingine ya Robo fainali itawakutanisha Stend United na Njombe Mji,mchezo ambao utapigwa kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

Mechi zote hizi zinatarajiwa kupigwa kati ya March 30 na Aprili 1 mwaka huu.

Michezo ya nusu fainali itazikutanisha mshindi wa timu hizi

Nusu Fainali
Stand United/Njombe Mji vs Azam FC/Mtibwa
Singida United/Young Africans vs Tanzania Prisons/JKT Tanzania
Fainali

Singida United/Young Africans vs Tanzania Prisons/JKT Tanzania vs Stand United/Njombe Mji vs Azam FC/Mtibwa.

No comments