YANGA WASEMA HAYA BAADA YA CHIRWA KUTAJWA KUJIUNGA NA SIMBA


Na Said Ally
Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kwamba mchezaji wao Obrey Chirwa ataendelea kusalia ndani ya klabu hiyo licha ya kuwepo kwa taarifa kutoka kwa baadhi ya wadau kueleza kuwa mchezaji huyo yuko mbioni kujiunga na mahasimu wao wa jadi Simba.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu ya Yanga Hussein Nyika alisema kwamba Obrey Chirwa ni miongoni mwa wachezaji ambao wanawahitaji kusalia ndani ya klabu hiyo,hivyo ni vigumu kumuacha aende katika klabu nyingine.

"Ni kwambie tu chukua neno kutoka kwangu kwamba mchezaji atakaeondoka kwenda Yanga labda sisi wenyewe Yanga tukubali yeye aondoke,lakini kama Yanga bado tunamuhitaji hakuna mtu ambae anaweza kumchukua"alisema Nyika.

Aidha Nyika alisema kwamba Chirwa alishindwa kuambatana na timu kwenda Shelisheli kwa kua alipata majeraha ya kuumia nyama za paja katika mechi ya Majimaji na wala hajagoma kama ambavyo inavyoelezwa na baadhi ya wadau.

Alisema kwamba baada ya kurejea kutoka Shelisheli Chirwa aliomba kuambatana na timu ili afanye mazoezi lakini daktari alishauri mchezaji huyo aendelee na matibabu kwa wiki moja.

Hata hivyo Nyika alithibitisha kuwa mkataba wa Chirwa unaelekea ukingoni kwa sasa lakini hilo halitomfanya yeye kuondoka kwenda klabu nyingine kwa kuwa benchi la ufundi linahitaji huduma yake na uongozi umepanga kumpa kandarasi mpya.

No comments