BAADA YA KUICHAKAZA NDANDA FC,YANGA YAWASILI JIJINI DAR ES SALAAM

Kikosi cha timu ya Yanga tayari kimewasili jijini Dar es salaam leo hii kikitokea mkoani Mtwara kilipokwenda kushiriki mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya  Ndanda FC ambapo katika mchezo huo Yanga ilifanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 2-1.

Afisa Habari wa Yanga,Dismas Ten ameiambia Saidallymwandike.blogsport.com kwamba kikosi kimewasili jijini Dar es salaam jioni ya leo tayari kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo wao wa klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

Ten alisema kwamba mipango yao kama uongozi ni kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika mechi hiyo ya klabu bingwa itakayopigwa march 6 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ili wajiwekee mazingira mazuri ya kutinga hatua ya makundi kwenye michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya vilabu barani Afrika.

No comments