JKT TANZANIA YAFANYA MABADILIKO YA MSEMAJI WA TIMU

Uongozi wa timu ya JKT Tanzania ambayo msimu ujao itashiriki ligi kuu ya Tanzania bara umetangaza rasmi kufanya mabadiliko ya afisa habari wa timu hiyo.

Aliyekuwa msemaji wa timu hiyo Costantine Masanja alisema kwamba kuanzia sasa afisa Habari wa timu hiyo atakuwa Luteni Seperatus Lubinga huku yeye akipewa majukumu mengine.

JKT Tanzania inayofundishwa na kocha Bakari Shime imedhamiria kufanya vizuri katika ushiriki wa michuano ya ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao huku pia wakiwa na mipango kabambe ya kuhakikisha wanatwaa taji la michuano ya kombe la FA ambayo inaendelea hivi sasa.

No comments