MECHI YA SIMBA KUCHEZWA USIKU,OKWI NA BOCCO WAKIWEMO

Na Mwandishi Wetu
Mtanange wa kimataifa  wa Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afika kati ya wekundu wa Msimbazi Simba na Al-Masry ya Misri  uliopangwa kuchezwa saa 10.00 jioni katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam sasa unatarajiwa kupigwa mishale ya saa 12.00 jioni kwa sasa hapa nyumbani Tanzania.

Mkuu wa idara ya Habari na mawasiliano wa Klabu ya Simba Haji Manara amesema kuwa wameamua kupeleka mda mbele wa mchezo huo kwasababu ni siku ya kazi na wamefanya hivyo ili kila Shabiki na mpenzi wa Simba aweze kwenda Uwanjani kuishuhudia Timu yao pendwa.

"Awali mchezo wetu ulipangwa kuchezwa saa 10.00 jioni lakini kutokana na heshima na kuwathamini Mashabiki wetu tumeona tuusogeze mbele mchezo huo ili mashabiki wetu wakitoka katika shughuli za kujiingizia kipato waje kuishangilia Timu yao pendwa"alisema Haji


Katika hatua nyingine Manara alisema kwamba kuelekea mchezo huo kwa upande wao matayarisho yamekamilika huku Al - Masry wakitarajiwa kuwasili siku ya kesho (Jumapili) na watafanya mazoezi jumatatu kwenye Uwanja wa Taifa ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa upande wao.

 Kwa upande wa Kikosi cha Simba tayari kimeingia Kambini leo hii kwenye Hotel ya SeaScape iliyopo Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo.

Manara ameongeza kuwa hali za wachezaji wao ambao ni majeruhi Bocco,Okwii na Haruna niyonzima wanaendelea  vizuri na jambo la faraja ni kuimalika kwa asilimia mia moja kwa wachezaji wao Okwi na Bocco ambapo anaamini kama watakuwa kwenye mipango ya mwalimu basi wachezaji hao wataonekana uwanjani.

"kwaupande wa wachezaji wetu ambao ni majeruhi Haruna ameisharudi kutoka India alikoenda kwa ajili ya matibabu na ametibiwa na ndani ya hizi siku mbili atajiunga na kikosi,kwaupande wa Bocco na Okwii wapo salama na tuliona tuwapumzishe"alisema Haji.

Hata hivyo Manara amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi katika pambano hilo kwa ajili ya kuipa sapoti timu huku pia akiwaomba mashabiki hao kuzipuuzia kebehi za Yanga wanazoendelea kuzitoa hasa baada ya kutoka sale ya 3-3 na Stend United kwenye mechi ya ligi kuu ya Tanzania bara iliyochezwa hapo jana kwenye uwanja wa Taifa.

No comments