MECHI YA YANGA NA MTIBWA SUGAR YAPIGWA KALENDA

Mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara kati ya Mtibwa Sugar na Yanga uliyopangwa kuchezwa march 3 mwaka huu umefanyiwa mabadiliko baada ya bodi ya ligi kupokea maombi kutoka katika klabu ya Yanga iliyoomba mechi hiyo isogezwe mbele ili ipate nafasi ya kujiandaa vizuri kwa ajili ya mechi yao ya klabu bingwa barani Afrika.

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniphace Wambura amesema kwamba mchezo huo sasa utapangiwa tarehe nyingine ambapo kwa kipindi hiki imewalazimu kuwapa fursa Yanga ili wajiandae na mechi yao klabu bingwa dhidi Township Rollers ya nchini Botswana.

Wambura alisema kwamba mbali na Yanga,pia mechi ya Simba na Stend United ambayo awali ilipangwa kuchezwa march 4 mwaka huu sasa itachezwa march 2 ili kuipa nafasi Simba ijiandae na mchezo wao wa kombe la shirikisho barani Afrika na hii imetokana na uongozi wa Simba kuomba mabadiliko ya mchezo wao huo.

No comments