KENYA NA UGANDA KULISHUHUDIA KOMBE LA DUNIA

Kombe halisi la dunia litakalokabidhiwa mshindi wa mashindano ya soka ya mwaka huu, yatakayofanyika nchini Urusi kati ya mwezi Juni linazuru maeneo mbalimbali duniani.
Utamaduni huu ulianza mwaka 2006, wakati fainali ya wakat huo ilipoandaliwa nchini Ujerumani.
Sudan imeshuhudia kombe hili kwa mara ya kwanza. Mwishoni mwa wiki iliyopita, wakaazi wa jiji la Khartoum walipata nafasi ya kulitazama kombe hilo na kupiga nalo picha.
Hata hivyo, marais wa nchi ambazo kombe hilo linazuru pekee ndio wanaoruhusiwa kulinyanyaua kombe hilo.
Baada ya kuwa nchini Ethiopia, siku ya Jumatatu na Jumanne, ni zamu ya nchi ya Kenya hasa jijini Nairobi, ambapo wapenzi wa soka watapata nafasi ya kupiga picha na kombe hilo na rais Uhuru Kenyatta kulinyanyua.
Kombe hili linazuru katika mataifa 10 pekee ya bara Afrika, ikiwa ni pamoja na Kenya, Uganda na Ethiopia, kutoka ukanda wa Afrika Mashariki.

No comments