TFF WAWEKA BAYANA JUU YA MABADILIKO YA MWAMUZI WA MECHI YA SIMBA NA AZAM FC
Na Said Ally
Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limekanusha taarifa zinazoeleza kuwa kamati ya waamuzi imefanya mabadiliko ya waamuzi katika mechi itakayowakutanisha Simba na Azam FC hapo kesho.
Afisa Habari wa TFF,Criford Mario Ndimbo ameiambia Saidallymwandike.blogspot.com kwamba katika mechi hiyo ya ligi kuu ya Tanzania bara hakuna mabadiliko yoyote ya waamuzi.
Alisema kwamba mechi hiyo itachezeshwa na mwamuzi Jonisia Rukya ambae alipangwa tangu awali akisaidiwa na Sudi Lila pamoja na Hereni Mduma atakaekuwa mwamuzi msaidizi namba mbili huku mwamuzi wa akiba akiwa Isihaka Mwalile.
Simba na Azam FC,hapo kesho zitamenyana katika uwanja wa Taifa katika mwendelezo wa ligi kuu ya Tanzania bara mzunguko wa pili ambapo mechi hiyo inatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu kwa pande zote.

Post a Comment