YANGA KUANZA UGENINI AZAM SPORTS FEDERATION CUP

Na Said Ally
Ratiba ya michuano ya mzunguko wa nne katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup imepangwa rasmi leo hii baada ya kufanyika droo ya kupata timu zitakazoshindana katika mechi hizo.

Katika droo hiyo iliyochezeshwa leo hii mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara Yanga watakuwa na kibarua kigumu cha kuwafuata wanalizombe wa Songea timu ya Majimaji.

Azam FC kwa upande wao watakuwa wageni wa timu ya KMC ambayo imekata tiketi ya kucheza ligi kuu ya Tanzania bara msimun ujao.

Singida United itakuwa nyumbani katika uwanja wao wa Namfua kuwakaribisha timu ya Polisi Tanzania.

Wakata miwa wa Manungu Turiani mkoani Morogoro,timu ya Mtibwa Sugar itawalazimu kusafiri hadi mkoani Geita kuwafuata mabingwa wa mkoa huo timu ya Buseresere ambayo hadi sasa ni timu pekee ya mabingwa wa mkoa waliosalia katika michuano hiyo.

Michezo mingine ni pamoja na
Stand United vs Dodoma FC
JKT Tanzania vs Ndanda FC
Kiluvya United vs Tanzania Prisons
Njombe Mji vs Mbao FC.

Mechi zote hizo za hatua ya 16 bora zitaanza kuchezwa kati ya Februari 22 na 25

No comments