YANGA YATIMULIWA UWANJA WA TAIFA


Na Said Ally
Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kwamba kikosi cha timu hiyo leo hii kimezuiwa kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Taifa wakati wakijiandaa na mchezo wao wa klabu bingwa barani Afrika dhidi ya St Louis kutoka nchini Ushelisheli.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu ya Yanga inaeleza kwamba klabu hiyo leo hii ilitaka kufanya mazoezi kwenye uwanja huo wa Taifa kwa sababu ndio utakaotumika kwa ajili ya mchezo wa huo wa kimataifa utakaopigwa siku ya jumamosi.

Kutokana na hali hiyo ya kuzuiwa kufanya mazoezi,iliwalazimu Yanga kwenda kufanya mazoezi katika uwanja wa chuo cha Polisi uliopo kurasini jijini Dar es salaam.

No comments