DAKTARI KUAMUA HATMA YA DONALD NGOMA

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kwamba kwa sasa wanasubiri lipoti ya daktari ili kufahamu hatma ya mchezaji Donald Ngoma aliye majeruhi kwa muda mrefu.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ndani ya klabu ya Yanga,Hussein Nyika alisema kwamba kwa sasa wanasubiri taarifa ya daktari ndani ya siku mbili hizi ili kutoa maamuzi ya uongozi wa klabu.

Alisema kwamba endapo kama taarifa zitaeleza kuwa Ngoma hatocheza kwa misimu miwili kuanzia sasa wao kama uongozi hawatakuwa na haja ya kuendelea nae zaidi ya kuvunja mkataba wake.

Hata hivyo Nyika alisema kwamba nchezaji huyo ameumia akiwa anaitumikia klabu hiyo hivyo ni vyema wakafuata taratibu sahihi hasa za kiutabibu kabla ya kuamua maamuzi yao.

No comments