SINGIDA UNITED WAMPUNGUZIA ADHABU KAMBALE

Na,Said Ally
Uongozi wa klabu ya Singida United umempunguzia adhabu mchezaji wao Kambale Salita Gentil ambae wiki moja iliyopita alisimamishwa kwa kosa la utovu wa nidhamu ndani ya uwanja.

Mkurugenzi wa ufundi wa Singida United Festo Richard Sanga alisema kwamba mchezaji Kambale alitii maelekezo ya klabu ya kuondoka kambini na kurejea Rwanda alikoweka makazi yake,zaidi mchezaji huyo aliiandikia klabu barua ya kujutia na kuomba msamaha kwa kosa alilotenda ili uongozi uweze kumpunguzia adhabu.

Sanga alisema kwamba uongozi umepokea ombi lake na unalenga kumpunguzia adhabu mchezaji huyo huku akiwa chini ya uangalizi wa maendeleo yake ya kinidhamu ndani na nje ya uwanja.

Kambale alisimamishwa na uongozi wa klabu ya Singida United baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wao wa kombe la FA walipocheza na timu ya daraja la pili Green Worriors ambapo alisababisha timu kucheza pungufu kutokana na kosa lake la kizembe.

No comments