YANGA YAWASILI SALAMA JIJINI MWANZA

Na Said Ally
Kikosi cha timu ya Yanga kimewasili salama jijini Mwanza tayari kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Mbao FC,hapo siku ya jumapili.

Kikosi hicho leo hii jioni kimefanya mazoezi yake katika uwanja wa Alliance na kesho wanataraji kukamilisha mazoezi yao katika uwanja wa CCM Kirumba tayari kwa mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.

Timu hiyo leo hii ilisafiri kwa ndege kuelekea jijini Mwanza kwa ajili mchezo huo ambapo pia baada ya mchezo  kikosi hicho kitasafiri kwa ndege kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kushiriki michuano ya kombe la mapinduzi.

No comments