SPORTPESA WAIPIGA TAFU POLISI TANZANIA

Kampuni ya inayojihusisha na michezo ya kubashiri ya SpotPesa imetoa Cheti cha Shukrani kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania; Simon Sirro kulishukuru Jeshi la Polisi kwa kuwa sehemu ya waliofanikisha ujio wa Everton nchin.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii mkurugenzi wa kampuni hiyo ya SportPesa  Abas Tarimba alisema kwamba mbali na cheti hicho pia wametoa hundi ya Sh. Milioni 20 na vifaa vya michezo kwa Timu ya Polisi Tanzania ili kuimarisha timu hiyo ikiwa ni moja ya utelekezaji wa SportPesa kwenye kuendeleza na kukuza Mpira wa miguu nchini.

Nae mkuu wa Jeshi la Polisi hapa nchini Simon Siro ameipongeza kampuni hiyo ya SportPesa kwa mchango huo ambao wameutoa akiamini kuwa utakuwa na tija kwa timu ya Polisi Tanzania hasa katika ushiriki wa ligi daraja la kwanza.

Alisema kwamba sapoti hiyo ambayo imetolewa na SportPesa itakua chachu ya timu ya Polisi Tanzania kupata nafasi ya kucheza ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao kwani wamejipanga kikamilifu.

No comments