SINGO AIKABIDHI BENDERA TIMU YA TANZANITE

Mkurugenzi wa michezo wa serikali Yusuf Singo leo hii ameikabidhi bendera timu ya Taifa ya vijana ya wanawake Tanzanite kwa ajili ya safari ya kuelekea nchini Nigeria kucheza mchezo wa kusaka tiketi ya kucheza kwa fainali za kombe la dunia.

Singo amewataka wachezaji hao ambao wataanza safari ya kwenda Nigeria usiku wa kuamkia kesho,kwenda kucheza kwa juhudi zaidi na kufanikiwa kuibuka na ushindi ili kuipa sifa nchi.

No comments