LAMECK NYAMBAYA AKABIDHI MIPIRA KWA VITUO VYA MKOA WA DSM

Mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF,Lameck Nyambaya leo hii amegawa mipira kwa wilaya tano za mkoa wa Dar es salaam kisoka kwa ajili ya maendeleo ya soka la vijana.

Nyambaya alisema kwamba TFF,imedhamiria kuhakikisha kunakua na umakini zaidi katika soka la vijana hivyo kwa upande wake kama mwakilishi wa mkoa wa Dar es salaam atalisimamia swala hilo kwa umakini zaidi.

Alisema kwamba mkoa huo umepewa mipira 200 kutoka TFF ambapo ameigawa katika wilaya tanohuku kila wilaya ikikabidhiwa mipira 40 itakayosaidia kwenye vituo mbalimbali vya kukuza vipaji.

Aidha alisema kwamba baada ya kubaini kua katika mkoa wake kuna upungufu mkubwa wa mipira ameamua kuchukua jukumu la kuongeza mipira 100 ili isaidie sehemu mbalimbali ikiwemo shuleni.

No comments