TFF WARIDHISHWA NA UWANJA WA AZAM COMPLEX

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limeridhishwa na hali ya uwanja wa klabu ya Azam FC,baada ya kuratibu vizuri pambano la ligi kuu ya Tanzania bara lililowakutanisha Azam FC na Simba.

Afsa Habari wa TFF,Alfred Lucas alisema kwamba shirikisho hilo linawapongeza wadau wote ambao wamehusika kufanikisha mchezo huo wa ligi kuu ya Tanzania bara unamalizika kwa amani na usalama wa hali ya juu.

Katika hatua nyingine shirikisho hilo la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limesema kwamba kwa kipindi hiki hawawezi kuidhinisha uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani utumike kwa ajili ya mechi za ligi kuu ambazo zitazihusisha timu za Simba na Yanga.

Lucas alisema kwamba TFF imechukua jukumu hilo baada ya kubaini uwanja huo wa Mabatini kutokizi vigezo vya kumudu kuhimili mashabiki wengi na kutokamilika kwa baadhi ya miundo mbinu ya uwanja.

No comments