YANGA WAPO KAMILI KUWAVAA MAJIMAJI

Uongozi wa timu ya soka ya Yanga umesema kwamba kikosi cha timu hiyo kipo vizuri kwa ajili ya mechi ya ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Majimaji itakayopigwa hapo kesho huko Songea.

Afsa Habari wa timu hiyo Dismas Ten amesema kwamba kiujumla hali ya kikosi iko vizuri kwa ajili ya pambano hilo ambalo linatarajiwa kua na ushindani wa hali ya juu.

Dismas alisema kwamba kwa sasa wanasubiri taarifa ya daktari wa timu ili kujua hatma ya nahodha msaidizi wa timu hiyo Thabani Kamusuko juu ya afya yake kama atamudu kucheza pambano hilo.

Alisema kwamba kiujumla hali ya wachezaji ukiondoa Kamusoko wote waliopo Songea wako vizuri kwa ajili ya mchezo huo wa ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments