MANJI AMJIA JUU PAULO MAKONDA KUHUSIANA NA TUHUMA ZA MADAWA YA KULEVYA

Baada ya kutajwa kwenye orodha ya watu wanatohumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paulo Makonda,mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuphu Manji amesema kuwa amefedheheshwa na kitendo hicho kwani kwa nafasi aliyo nayo kwa jamiii si vyema kwa yeye kutuhumiwa kwa jambo hilo.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii,Manji amesema kwamba yeye ni miongoni mwa watu ambao wanaongoza taasisi kubwa ikiwemo klabu ya Yanga hivyo kupewa tuhuma hizo kupitia vyombo vya habari si utaratibu sahihi.

Alisema kwamba katiba inaeleza kuwa kila mtu ana haki yake,hivyo kumchafua yeye ni sawa na kuichafua klabu ya Yanga kwa kuwa yeye ndie mwenyekiti wa klabu hiyo.


Hata hivyo amedai kuwa yeye siku ya kesho ataenda kulipoti Polisi na wala hatasubiri hiyo siku ya ijumaa kama alivyoagizwa na Makonda kwa sababu hawezi kubadili ratiba yake ili akae foleni ya watu 65.

No comments